Ndugu yetu mpendwa,
Inaruhusiwa kuweka majina yenye maana nzuri kwa Kifarsi au lugha nyingine. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alibadilisha majina yasiyofaa kwa Uislamu. Hii ni sunna. Lakini, Mtume wetu (saw) hakuamrisha Waislamu kubadilisha majina yao ya zamani, wala hakuamrisha watu wasio Waarabu waliokuwa wameingia katika Uislamu kuchukua majina ya Kiarabu, bali aliamrisha tu kwamba majina yatakayopewa yawe na maana nzuri. Alibadilisha baadhi ya majina kwa sababu ya maana zake mbaya, na baadhi ya majina mengine yenye maana nzuri sana aliyabadilisha kwa sababu ya matumizi mabaya yaliyoweza kuleta maana mbaya au kuleta athari mbaya kwa mwenye jina.
Bonyeza hapa kwa maelezo zaidi:
Ni nini kinachohitajika kufanywa kwa mtoto mchanga; ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kumpa jina?
Salamu na dua…
Uislamu kwa njia ya maswali