Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Siku moja, malaika wanne wakuu wa Mwenyezi Mungu walinijia. Hao ni Jibril, Mikail, Israfil na Azrail (alayhimus-salam). Jibril (alayhis-salam) akaniambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtu yeyote katika umma wako akikusalia mara kumi kwa siku, kesho siku ya kiyama nitamshika mkono na kumvusha Sirati kama ndege. Mikail (alayhis-salam) naye akasema: Mimi nitamnywesha yule mja maji ya kutosha kutoka kwenye kisima chako cha Kawthar. Israfil (alayhis-salam) akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kwa ajili ya msamaha wa yule mja, nitasujudu na sitainua kichwa changu mpaka Mwenyezi Mungu amsamehe. Azrail (alayhis-salam) naye akasema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu! Mimi nitamchukua roho ya yule anayekusalia mara kumi kwa siku kama vile ninavyochukua roho za Mitume.” Baada ya hapo, Mtume wa Mitume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Hii ni neema kubwa mno, Ewe Mola wangu! Hii ni ihsani kubwa mno, Ewe Mwenyezi Mungu!”
Ndugu yetu mpendwa,
Mada hii imehamishwa pamoja na majibu na maoni yake, bofya hapa ili kusoma…
Salamu na dua…
Uislamu kwa njia ya maswali